Trump aingilia masuala ya ndani ya Uingereza kwa 'kumponda' Corbyn kuwa hafai kuwa waziri mk


Katika kile kinachoonekana kuwa ni uingiliaji wa masuala ya ndani ya Uingereza, Rais Donald Trump wa Marekani amesema, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Leba, Jeremy Corbyn si chaguo mbadala linalofaa kwa uwaziri mkuu wa nchi hiyo.

Akizungumza katika mahojiano na redio ya LBC Trump amesema, Corbyn hana uwezo wa kuiongoza Uingereza; na kwa mara nyingine akatangaza uungaji mkono wake kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson.

Matamshi hayo ya Trump ya kuingilia masuala ya ndani ya Uingereza yametolewa wakati ambao, hapo jana, katika mkutano wake wa kwanza wa kampeni za uchaguzi wa kabla ya wakati, kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn alitoa maneno makali dhidi ya Johnson na Trump.

Katika mkutano wake huo wa kampeni, Corbyn aliahidi kuwa ataitisha kura ya pili ya maoni ya Brexit na kuyafuta makubaliano ya kibiashara anayopigania rais wa Marekani yafikiwe kati ya nchi hiyo na Uingereza.

Siku ya Jumatano ya tarehe 30 Oktoba, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alipata ridhaa ya Bunge la nchi hiyo ya kuitisha uchaguzi wa kabla ya wakati mnamo tarehe 12 Desemba mwaka huu.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu