Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mgogoro wa Fizi jimbo la Kivu Kusini

November 1, 2019

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu machafuko ya kikabila ambayo yanaweza kutokea katika eneo la Fizi jimboni Kivu ya kusini ambako makundi ya wapiganaji wa kikabila yameendesha mashambulizi kwa zaidi ya miezi 6.

 

Kwenye mkutano na wandishi habari hapa mjini Kinshasa,kiongozi wa tume ya haki za dinadamu ya umoja wa mataifa nchini Kongo, Abdoulaziz Thioye amesema kwamba hali ya kiusalama kwenye mtaa wa Fizi, huko Kivu ya kusini, nilazima iboreshwe haraka iwezekanavyo.

 

Thioye amesema kwamba miito kwa ajili ya kuchochea chuki za kikabila inahatarisha amani kwenye eneo hilo

 

"Machafuko hayo ambayo yametokea huko Minembwe toka mwezi wa machi, kuna mameno ya uchochezi wa chuki yanano ripotiwa baina ya jamii zinazohasimia. Tumeshuhudia pia chuki za kikabila na hata uraia wa Kongo, hali hiyo inaleta tatizo.Kunaumuhimu wa kurejesha kila mutu kwenye jia ya busara,wakiwemo wale wanaochochea kisisisiri machafuko hayo,na mabao ni watu wanaoshikilia madaraka kwa ngazi ya juu," alisema Abdoulaziz Thioye

 

Umoja wa mataifa unaelezea kwamba zaidi ya vijiji 73 vimechomwa moto na makundi ya wapiganaji wa kikabila. Huku vijiji 4 ambavyo ni vya jamii ya kabila la Benyamulenge.

Wazalia wa Kivu ya kusini wanaoishi hapa mjini Kinshasa,wameanzisha juhudi za upatinishi ilikumalizisha machakufuko hayo. Norbert Basengezi, alienazisha mazungumzo ya makundi ya kikabila kutoka mtaa wa Fizi.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload