Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi yatangaza kuwaunga mkono waandamanaji Iraq

November 1, 2019

Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya nchi Iraq imetangaza kuwa, haiingilii masuala ya kisiasa nchini humo lakini inaunga mkono matakwa halali ya wananchi kupitia maandamano ya amani.

 

Taarifa iliyotolewa na harakati hiyo imesisitiza kuwa, Hashdu sh-Sha'abi inaunga mkono matakwa ya waandamanaji lakini kamwe haiingilii masuala ya kisiasa ya nchi hiyo, kwa kuwa harakati hiyo ni sehemu ya askari wa kusimamia usalama na kulinda umoja wa Iraq. Aidha imeongeza kwamba, wadhifa wake ni kulinda usalama wa nchi na wananchi mbele ya magaidi. 

 

Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi  imeongeza kwamba baadhi ya mitandao ya kijamii inafanya njama za kueneza taarifa tofauti za upotoshaji dhidi yake ambapo taarifa ya karibuni kabisa ni habari ya upotoshaji kwamba magari ya kijeshi ya Hashdu sh-Sha'abi yaliyopo katika ofisi ya Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa harakati hiyo eneo la Jadiriyah, zilihusika katika ukandamizaji wa waandamanaji.

Katika taarifa hiyo, harakati hiyo imesema kuwa ofisi ya al-Muhandis haipo eneo la Jadiriyah na kwamba ofisi yake ipo eneo la makao makuu ya Hashdu sh-Sha'abi huko Green Zone mjini Baghdad.

 

Hii ni katika hali ambayo ofisi ya Ayatullah Sayyid Sistan, marjaa wa Waislamu wa Shia nchini Iraq imetangaza pia kuunga mkono maandamano ya amani ya wananchi kwani maandamano hayo ni haki yao ya kimsingi.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon