Pande hasimu Syria zakutana Geneva kwa mazungumzo

October 31, 2019

Pande hasimu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane na nusu zimekutana Jumatano mjini Geneva, Uswisi, wakijaribu kutunga katiba mpya kumaliza vita.

Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Katiba ya Syria kutoka upande wa Serikali Ahmad Kuzbari, amesema mchakato huo utafanikiwa pindi kila upande utakuwa na nia njema kwa maslahi ya nchi yao.

 

"Inazingatiwa kuwa ni mchakato wa kisiasa wa kumaliza mzozo ambao umeharibu nchi yetu. Mchakato huu unaweza kufanikiwa kwa dhamira thabiti na uamuzi dhahiri wenye imani njema pamoja na kufanya bidii kuhifadhi umoja, na uhuru wa nchi yetu. Kuhakikisha haki za watu wetu na ujasiri na nguvu ya nchi yetu," amesema Kuzbari.

 

Lakini wataalamu wanahoji iwapo serikali ya Rais Bashar al-Assad itakuwa tayari kukubali mengi yatakayojadiliwa katika meza ya mazungumzo baada ya jeshi lake kuchukua udhibiti mkubwa wa ardhi nchini humo.

 

Urusi na Iran, washirika wa serikali ya Syria pamoja na Uturuki inayounga mkono upande wa upinzani, wanauangalia mkutano huo wa Kamati ya Katiba kama fursa ya kujenga imani miongoni mwa pande zote na kusaficha njia kuelekea mchakato mpana zaidi wa kisiasa ambao utaweza kumaliza mgogoro huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amezihimiza pande zote husika kufikia makubaliano.

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema nchi hizo washirika hazitoingilia mchakato huo, na mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema ana matumaini lakini pia anafahamu kuwa mazungumzo hayo yatakuwa magumu.

 

www.mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon