Wanajeshi wa Kizayuni waendelea kubomoa nyumba za Wapalestina


Wanajeshi wa utawala haramu wa Kizayuni kwa mara ya 165 wameendelea kubomoa kijiji cha al Araqeeb kinachokaliwa na jamii ya Mabedui katika eneo la Naqab linalokaliwa kwa mabavu.

Jeshi la utawala wa Kizayuni jana Jumanne huku likiwa na mabulzoda na idadi kubwa ya wanajeshi lilikivamia na kuanza kubomoa nyumba za wenyeji wa kijiji cha al Araqeeb katika ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 1948.

Baada ya kufanya uharibifu huo katika kijii cha al Araqeeb, wanajeshi hao ghasibu walimtia mbaroni pia Sheikh Sabah Turi kiongozi wa kijiji hicho. Utawala wa Kizayuni tangu mwaka 2000 hadi sasa umekivamia mara 165 kijiji hicho cha Mabedui cha al Araqeeb hata hivyo wakazi wa kijiji hicho hakuna siku waliyokata tamaa na kila siku wamekuwa wakikijenga upya kijiji chao hicho na hawako tayari kukihama.

Duru za kimataifa mara kadhaa zimewasilisha wito zikitaka kusimamishwa bomoabomoa hiyo dhidi ya kijiji hicho cha Mabedui hata hivyo utawala wa Kizayuni unaendelea kuwafanya wakimbizi wakazi wa kijiji hicho kwa kupuuza matakwa hayo ya kimataifa.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu