Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Watu wasiopungua 22 waaga dunia katika maporomoko ya udongo yaliyoiathiri Cameroon

October 30, 2019

Timu ya wafanyakazi wa huduma za uokoaji jana walikuwa wakipekua vifusi vya nyumba za manusura baada ya maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa kuua watu wasiopungua 22.

 

Polisi pia wamekuwa wakiwasaka makumi ya watu wengine walioripotiwa kutoweka katika mji wa Bafoussam katika miinuko ya magharibi umbali wa kilomita 200 kaskazini mwa mji wa bandari kuu wa Doaula. Awa Fonka Augustine Gavana wa mkoa wa Magharibi nchini Cameroon amesema kuwa ni wazi kuwa, wakazi wa eneo hilo wanapasa kuondoka katika makazi yao kwa kuzingatia kuweko uwezekano wa kujiri maafa zaidi.

Mvua kubwa zimeendelea kunyesha nchini Cameroon na hivyo kusababisha mafuriko yaliyowafanya watu karibu elfu 30 kukosa makazi.

 

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) wiki iliyopita liliripoti kuwa, mvua zisizo za kawaida zilizoikumba Sudan Kusini pia zimebomoa vituo vya afya na barabara na kufanya huduma za chakula na maji kwa watu karibu milioni moja kuwa ngumu zaidi.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload