Shambulizi dhidi ya msikiti Ufaransa; watu wawili wapigwa risasi


Watu wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi nje ya msikiti mmoja katika mji wa Bayonne, kusini magharibi mwa Ufaransa.

Vyombo vya usalama nchini humo vimesema kuwa vimemtia mbaroni mzee wa miaka 84 mwenye chuki dhidi ya Uislamu na Uislamu kwa jina Claude Sinke, anayetuhumiwa kuwapiga risasi wawili hao walipomkuta akijiandaa kuuteketeza moto Msikiti wa Bayonne, baada ya kulichoma moto gari lililokuwa limeegeshwa nje ya msikiti huo.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amelaani shambulizi hilo la jana alililolitaja kuwa la kihaini, na kusisitiza kuwa serikali yake itafanya kile iwezalo kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wengine wa jinai hiyo, huku akiwahakikishia usalama 'Waislamu wazalendo'.

Hii ni katika hali ambayo, Jumapili iliyopita, miji kadhaa ya Ufaransa ukiwemo mji mkuu Paris, Marseille, Lyon na Metz ilishuhudia mikusanyiko mikubwa ya kulaani na kulalamikia ubaguzi na chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.

Jumuiya ya kukabiliana na uenezaji wa hisia za chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa, Jumuiya ya Haki za Binadamu za Waislamu na misikiti kadhaa ya Ufaransa ndizo zilizoandaa na kuratibu mikusanyiko hiyo.

Wimbi la chuki dhidi ya Uislamu na kampeni za kuichafua dini hii limeongezeka mno barani Ulaya na Marekani katika miaka ya hivi karibuni.

ww.w.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu