Siku 6 za kuweka chini silaha zinamaliza nchini Syria

October 29, 2019

Makubaliano yaliokwama ya siku 6 kusitisha mapigano kati ya Uturuki na Urusi ambayo yalilenga kutoa nafasi kwa wanamgambo wa Kikurdi wa YPG kuondoka eneo la kaskazini mashariki mwa Syria yanafikia mwisho (29.10.2019).

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalipaswa kuanza kutekelezwa Oktoba 22  takribani majuma mawili baada ya serikali ya Uturuki kuanzisha mashambulizi makali ya kijeshi dhidi ya kundi hilo,yaliyokosolewa  na  mataifa  kadhaa ulimwenguni. Kwa mujibu wa makubaliaono haya wapiganaji wa kundi la YPG lilipaswa kuwa na muda hadi wa saa 12 jioni ya leo  kuondoka katika  Kaskazini Mashariki mwa Syria.

 

Kundi la wanamgambo wa YPG,ndio lilikuwa jeshi lenye kutegemewa katika vita ya ardhini katika kukabiliana na Kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria, ambalo lilikuwa linaungwa mkono na mataifa ya magharibi na vikosi maalumu. Lakini serikali ya Uturuki inaliunganisha kundi hilo na lile la Uturuki la chama PKK, ambalo wao, Uturuki, Umoja wa Ulaya na hata Marekani.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amerudia mara kadhaa kutoa kutishia kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao ikiwa hawajaondoka kwenye eneo hilo kufikia muda wa mwisho uliowekwa.Jana waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu alisistiza onyo lililotolewa na rais Erdogan.

 

Urusi imelipa onyo kundi hilo kwamba majeshi yake na ya Syria yameweka kambi kwa muda katika eneo hilo ili kuweza kuhakiki, hatua ya uondokaji na salama kwa kutoa ulinzi.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon