Jeshi la Lebanon latahadharisha kuhusu fitina na njama mpya za MOSSAD

October 29, 2019

Jeshi la Lebanon limetoa taarifa likitangaza kuwa, ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook unaofanya kazi chini ya usimamizi wa shirika la ujasusi la Israel MOSSAD kwa kutumia jina la "Jamal Fa" unatuma maombi na kutoa pesa kwa baadhi ya raia wa Lebanon.

 

Katika taarifa hiyo jeshi la Lebanon limewataka raia wa nchi hiyo kuwa macho na makini ili wasitumbukie katika mtego wenye lengo la kuchochea moto wa fitina na machafuko nchini humo.

Itakumbukwa kuwa sheria iliyopasishwa nchini Lebanon tarehe 23 Juni mwaka 1955 inawapiga marufuku raia wote wa nchi hiyo kuwa na uhusiano na utawala haramu wa Israel.

 

Wakati huo huo Wizara ya Afya ya Lebanon imetahadharisha kuhusiana na uhaba wa dawa nchini humo kutokana na kuendelea kufungwa barabara na benki na kuzuiliwa madawa katika idara za forodha za nchi hiyo

Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa, hatua ya waandamanaji ya kuendelea kufunga barabara imesababisha uhaba wa dawa katika maduka mengi ya kuuza bidhaa hiyo na kwamba mahospitali pia yanakabiliwa na matatizo mengi.

Tangu Alkhamisi iliyopita Lebanon imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia ushuru uliowekwa na serikali na hali mbaya ya uchumi.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon