Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

mapambano ya Iran dhidi ya magendo ya mafuta

July 19, 2019

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC au SEPAH limetangaza kwamba limetumia kibali cha mahakama kusimamisha meli moja iliyokuwa imebeba mafuta ya magendo katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

 

Jeshi hilo jana Alhamisi baada ya kuhakikisha kwamba meli moja ya kigeni ilikuwa imebeba lita milioni moja za mafuta ya magendo, na kupata kibali kutoka kwa maafisa husika wa vyombo vya mahakama vya humu nchini, lililazimika kuisimamisha meli hiyo kusini mwa Kisiwa cha Larak katika Ghuba ya Uajemi. Hatua hiyo ya SEPAH imetekelezwa katika fremu ya majukumu yake mazito ya kulinda usalama katika maji ya Ghuba ya Ujemi na Lango Bahari la Hormoz.

 

Jukumu kuu la jeshi hilo la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo hilo, ni kulinda maslahi ya taifa la Iran, usalama na kupambana na magendo ya baharini. Kwa mujibu wa Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, jeshi hilo, ikiwa ni katika kutekeleza jukumu lake la kupambana na magendo ya mafuta, kila siku huchukua hatua kama vile za kusimamisha meli zinazobeba mafuta ya magendo katika Ghuba ya Uajemi.

Licha ya kuwa magendo ya mafuta yanahatarisha maslahi ya taifa la Iran pia yanachukuliwa kuwa ni changamoto muhimu ya kimataifa.

 

Kitendo cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha kusimamisha meli hiyo ya kigeni iliyokuwa imebeba mafuta ya mgendo licha ya kuwa ni utekelezaji wa jeshi hilo wa majukumu yake ya kitaifa pia ni alama ya uwajibikaji wake katika kulinda usalama wa mkondo wa kudhamini nishati ya kimataifa.

 

Hatua hiyo imetekelezwa kikamilifu katika fremu ya sheria za ndani ya nchi na vilevile za kimataifa kuhusiana na masuala ya ubaharia na safari za baharini.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload