Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mahakama ya Nigeria yachunguza uwezekano wa kuruhusiwa Sheikh Zakzaky kutibiwa nje ya nchi

July 19, 2019

Duru za kieneo zimetangaza kuwa, Mahakama Kuu ya Nigeria inachunguza uwezekano wa kuruhusiwa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongbozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo kwenda kutibiwa nje ya nchi.

 

Duru za kieneo nchini Nigeria zimesema kuwa, Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna jana Alkhamisi iliitisha kikao cha kusikiliza kesi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na mawakili walimwambia jaji wa mahakama hiyo kwamba, kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria pamoja na mambo mengine, anasumbuliwa pia na maradhi ambayo yanamfanya asiweze kupanda ngazi za mahakamani hapo, hivyo amelazimika kubakia nje ya mahakama.

 

Mawakili hao wameiomba mahakama iruhusu Sheikh Zakzaky na mkewe waende wakatibie nchini India na mahakama hiyo nayo imeahidi kulitolea uamuzi ombi hilo katika kikao kijacho cha siku ya Jumatatu.

 

Mwaka 2015, jeshi la Nigeria lilivamia na kushambulia mkusanyiko wa Waislamu katika Husainia ya Zaria kwenye jimbo la Kano na kuua shahidi kwa umati karibu Waislamu elfu moja akiwemo mtoto wa kiume wa Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Baadhi ya madaktari wa kigeni waliomtembelea Sheikh Ibrahim Zakzaky jela na kuchunguza afya yake.

 

Sheikh Zakzaky mwenyewe na mkewe walipigwa risasi na tangu wakati huo wanashikiliwa katika korokoro za serikali ya Rais Muhammadu Buhari ambayo inaendelea kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya kumwachilia huru mwanachuoni huyo.

 

Ripoti mbalimbali za uhakika zinasema kuwa hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky ni mbaya na hata damu yake imegunduliwa kuwa na chembe chembe za risasi kutokana na mateso anayopewa huku hali yake na mkewe ikizidi kuwa mbaya, siku baada ya siku.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload