Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Wawakilishi wa Baraza la Kijeshi Sudan na muungano wa upinzani wasaini makubaliano ya kisiasa

July 18, 2019

 Wawakilishi wa Baraza la Kijeshi la uongozi wa mpito nchini Sudan na muungano wa upinzani leo Jumatano wamesaini makubaliano ya kisiasa kama sehemu ya kugawana madaraka kwa lengo la kuielekeza nchi hiyo kwenye demokrasia.

 

Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Khartoum mbele ya wapatanishi kutoka nchi kadhaa za Afrika kufuatia mazungumzo ya usiku kucha ili kufanikisha baadhi ya masuala yaliyokuwa yamesalia.

 

Ibrahim al Amin wa muungano wa wapinzani wa Uhuru na Mabadiliko  amesema baada ya kusainiwa makubaliano hayo ya kisiasa kuwa wanataka kuona nchi yao ikiwa na amani kwa sababu wametaabika sana.

 

Mpatanishi kutoka Ethiopia, Mahmud Dirir amesema kuwa Sudan inahitajia kupambana na umaskini na ametoa wito wa kuondolewa nchi hiyo katika orodha ya Marekani ya nchi zinazounga mkono ugaidi.

Wajumbe baada ya kusiani makubaliano ya kisiasa Sudan 

 

Habari kutoka Khartoum zinasema kuwa pande mbili hizo zilizosaini makubaliano hayo ya kisiasa zingali zinaendelea kujadili suala la kutoa tangaza la kikatiba ambalo linatazamiwa kusainiwa Ijumaa kesho kutwa. Baraza la Kijeshi la Sudan lilichukua madaraka tarehe 11 Aprili mwaka huu baada ya jeshi la nchi hiyo kumpindua Omar Hassan al-Bashir.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload