Makundi matatu ya waasi yaweka chini silaha zao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

July 18, 2019

Makundi matatu ya wabeba silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamekabidhi silaha zao kwa wawakilishi wa Umoja wa Mataifa.

 

Makundi hayo ya waasi yaliyokuwa yakiendesha harakati zao magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, jana Jumatano yalikabidhi silaha zao kwa ujumbe wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA.

 

Imeelezwa kuwa, hatua hiyo ni utekelezaji wa mpango wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ulioanza kutekelezwa Disemba mwaka jana wa upokonyaji silaha, kuondoka makundi ya wabeba silaha katika harakati za uasi na kuunganishwa tena na nchi.

 

Aidha mpango huo ni utekelezaji wa upokonyaji na uwekaji chini silaha makundi 14 ya wabeba silaha yaliyotia saini makubaliano ya amani na serikali ya Bangui.

Askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA)

 

Licha ya kupata miezi kadhaa tangu kutiwa saini makubaliano hayo, lakini hadi sasa athari ya makundi yaliyotia saini makubaliano hayo huko Khartoum Sudan hayatekelezi ahadi ya kuweka chini silaha na kuacha uasi.

 

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa mwaka 2013 baada ya kuondolewa madarakani Rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé kufuatia hujuma ya waasi. 

 

Tangu wakati huo hadi sasa nchi hiyo imekuwa uwanja wa mapigano ya kila uchao kati ya makundi hasimu, hususan lile la Kikristo la Anti-Balaka na lile la Seleka. Hali hiyo imezidi kuisababishia matatizo mengi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon