Bajeti mpya ya serikali ya Marekani kwa wapinzani wa serikali ya Venezuela

July 18, 2019

Serikali ya Marekani imepanga kuwapatia wapinzani wa serikali nchini Venezuela bajeti ya zaidi ya dola milioni 40 kwa ajili ya kuendeshea harakati zao.

 

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) limeitaarifa Kongresi ya nchi hiyo kwamba itawapatia wapinzani wa serikali ya Venezuela bajeti ya dola milioni 40.

 

Bajeti hiyo itakabidhiwa kwa Juan Guaido kiongozi wa wapinzani wa Venezuela na makundi mengine yanayomuunga mkono.

 

Aidha imeelezwa kuwa bajeti ya dola milioni 40 itatolewa pia kwa Guatemala na Honduras ili eti ziweze kukabiliana na changamoto kama umaskini na machafuko. 

 

Rais Donald Trump wa Marekani mwaka jana alitangaza kuwa atasitisha misaada ya kifedha kwa nchi za Amerika ya Kati iwapo viongozi wa nchi hizo hawatazuia wimbi la wahajiri kuelekea Marekani.

 

Serikali ya Marekani ingali inaendelea kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Venezuela.

Juan Guaido, kiongozi wa wapinzani Venezuela


Kiongozi wa wapinzani nchini Venezuela Juan Guaido mwishoni mwa Aprili mwaka huu alifanya jaribio la mapinduzi ambalo liligonga mwamba baada ya kuzimwa vikali na jeshi na wananchi wa Venezuela. Jaribio hilo lilifanyika kwa msaada wa Marekani na waitifaki wake.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon