Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Wanamgambo 15 wa kundi la kigaidi la al-Shabab waangamizwa na jeshi la Somalia

July 15, 2019

Jeshi la Somalia limetangaza kuwa, limewaangamiza wanachama 15 wa kundi la kigaidi la al-Shabab katika operesheni ya jeshi hilo katika siku za hivi karibuni.

 

Mtandao wa al-Yaum Sabi'i umewanukuu maafisa wa jeshi la Somalia wakitangaza hiyo jana kwamba, wanachama hao wa al-Shabab wameuawa katika operesheni ya kijeshi iliyofanywa katika mkoa wa Lower Shabelle. Taarifa ya jeshi la Somalia imeeleza pia kuwa, wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuvikomboa vijiji viwili katika mkoa huo vilivyokuwa vikidhibitiwa na wanamgambo hao.

 

Wakati huo huo, maafisa wa serikali ya Somalia wametangaza kuwa, operesheni ya jeshi la nchi hiyo itaendelea katika mkoa wa Lower Shabelle hadi pale jeshi litakapofanikiwa kuwatimua kikamilifu wanamgambo wa al-Shabab katika mkoa huo.

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabab

 

Hayo yanajiri siku chache tu baada ya watu wasiopungua 26 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mji wa bandari wa Kismayo kufuatia shambulio la kigaidi ambapo gaidi mmoja aligongesha gari lililosheheni mada za milipuko katika Hoteli ya Asasey  kabla ya washambuliaji hao kuvamia jengo hilo.

 

Somalia iliyoko katika Pembe ya Afrika ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 na katika miaka ya hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wakufurishaji wa al-Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload