Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Trump awatukana matusi ya kibaguzi wabunge wanawake wa Kongresi ya Marekani

July 15, 2019

Rais Donald Trump wa Marekani amewatukana matusi ya kibaguzi wabunge wanawake wa chama wa Democrat katika Kongresi ya Marekani kwa kuwaambia, wao si Wamarekani na kuwataka warudi katika nchi walizotoka.

 

 

Trump ametoa matusi hayo ya kibaguzi kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika ujumbe usemao:

 

"Ni jambo la kuvutia mno kuona wabunge wanawake 'wapenda maendeleo' wa Democrat katika Kongresi, ambao kimsingi wamekuja kutoka nchi ambazo serikali zao ni majanga matupu, zikiwa ni miongoni mwa serikali mbaya zaidi, fisadi zaidi na mbovu zaidi duniani (kwa sharti kama hizo serikali zenyewe zitakuwepo katika nchi hizo), sasa wanawapazia sauti  na kwa ukali wananchi wa Marekani, ambayo ni nchi kubwa zaidi na yenye nguvu zaidi duniani, kuwaambia ni vipi serikali yetu inapasa iendeshwe."  

 

 

Katika ujumbe wake huo, Trump ameongezea kwa kusema: "Kwa nini hawarudi na kwenda kusaidia kurekebisha maeneo walikotoka yenye uhalifu? Kisha rudini muje kutuonyesha vipi mumeifanya kazi hiyo. Sehemu hizo zinahitaji sana msaada wenu. Inapasa muondoke haraka iwezekanavyo."

 

Kutoka kushoto: Ilhan Omar, Ayanna Pressley, Alexandria Ocasio-Cortez na Rashida Tlaib

 

Japokuwa hakuwataja kwa majina, wabunge wanawake aliowalenga Trump kwa matamshi hayo ya chuki za kibaguzi ni Ilhan Omar aliyezaliwa Somalia, RashidaTlaib mwenye asili ya Palestina, Alexandria Ocasio-Cortez ambaye asili yake ni Puerto Rico na  Ayanna Pressley, Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload