Kansela wa Ujerumani asisitizia ulazima wa kuacha kuiuzia silaha Libya

July 11, 2019

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesisitiza kupatikana njia ya kidiplomasia kwa ajili ya kuutatua mgogoro wa Libya na kuitolea wito jamii ya kimataifa kuacha kuiuzia silaha nchi hiyo.

 

 

Angela Merkel amelaani mashambulizi dhidi ya kituo cha kuhifadhia wakimbizi huko Libya na kutaka kutekelezwa usitishaji vita nchini humo bila ya masharti yoyote.

 

Merkel ameashiria uanachama wa Ujerumani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi hiyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwazo ya Libya na kueleza kuwa:

 

Wale wote ambao walikuwa nje ya nchi wamepeleka silaha nyingi huko Libya; na ndio maana inapasa wawekewe vikwazo vya silaha ili kuweza kukabiliana zaidi na hatua yoyote inayozusha machafuko.  

 

Duru mpya ya mapigano huko Libya ilianza tangu Aprili mwaka huu kwa kufanywa mashambulizi huko Tripoli na wanamgambo wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na kamanda Khalifa Haftar; mashambulio ambayo yalijibiwa na vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Fayez al Siraj. 

Kamanda Khalifa Haftar

 

Kundi hilo la jeshi la kitaifa la Libya limeshindwa kuudhibiti mji mkuu Tripoli licha ya kuungwa mkono kisilaha na kifedha na Imarati, Saudi Arabia, Misri na vile vile Ufaransa.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon