Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Balozi wa Uingereza Washington ajiuzulu baada ya kushambuliana kwa maneno na Trump

July 11, 2019

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza imetangaza kuwa balozi wa London mjini Washington Kim Darroch, amejiuzulu kufuatia mzozo wa kushambuliana kwa maneno uliojiri baina yake na Rais Donald Trump wa Marekani.

 

 

Wizara hiyo imetangaza kuwa, Trump alikata mawasiliano ya aina zote na Kim Darroch baada ya kuvuja barua za siri za  balozi wa Uingereza huko Washington zilizoweka wazi matatizo na kupoteza uelekevu  wa Rais Donald Trump pamoja na serikali yake.

 

Kim Darroch katika ripoti ya siri aliyoituma kwa serikali ya Uingereza, alimtaja Trump kuwa mtu duni na asiye na weledi wa diplomasia.

 

Aidha alitabiri kuwa kipindi cha urais cha Trump kitaishia kwa rais huyo kukabiliwa na kashfa na kwamba hatamaliza muhula wake wa uongozi.

 

Sir Darroch alituma barua hizo kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingeza ambapo aliashiria kauli za kashfa zinazotolewa na Donald Trump na kueleza kwamba, kwa hali hii haiyumkiniki kuweza  kuendelea kutekeleza majukumu yake kama rais.

Sir Kim Darroch, Balozi wa Uingereza mjini Washington aliyejiuzulu

 

Jumanne usiku Trump aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuhusu Kim Darroch kwamba: "Balozi aliyechanganyikiwa, ambaye Uingereza imemtuma Marekani ni mtu mpumbavu sana. Sisi hatutashirikiana naye tena".

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload