Uingereza kuchunguza kuvuja kwa maoni ya Balozi wake dhidi ya rais wa Marekani


Balozi Kim Darroch

Serikali ya Uingereza imesema inapanga kuchunguza kuvuja kwa jumbe za siri ambapo balozi wake nchini Marekani ameuita utawala wa rais Donald Trump usio na ujuzi wala stadi za kuongoza.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza amesema uchunguzi kuhusu kuvuja kwa jumbe hizo kupitia gazeti la Mail utaanzishwa.

Katika mfululizo wa jumbe hizo za kuanzia mwaka 2017 hadi karibuni, balozi Kim Darroch amedai kuwa Ikulu ya Marekani ''haiwezi kufanya kazi ipasavyo'' na ''imegawanyika'' chini ya utawala wa Trump.

Pia amesema rais wa Marekani ameonesha kukosa utulivu na usalama katika wadhifa wake.

Rais Trump amemkosoa balozi Darroch kwa kusema utawala wake hauridhishwi na kazi anayofanya na kwamba mwanadiplomisia huyo haijaiwakilisha vyema Uingereza nchini Marekani.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu