Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Maandamano ya wahajiri wa Ethiopia mjini Haifa, kupinga ukatili na ubaguzi wa rangi wa utawala wa Israel

July 6, 2019

Jamii ya wahajiri wa Ethiopia wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel, imeisababishia changamoto mpya serikali ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo, kutokana na maandamano yake mapya mjini Haifa.

 

 

Hata kama sababu ya maandamano ya sasa ya wahajiri hao wa Ethiopia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu inatokana na kuuawa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 na polisi wa utawala haramu wa Israel, lakini maandamano ya wahajiri hao wanaoishi huko Israel sio suala jipya na lina sababu za msingi.

 

Kwa mujibu wa takwimu, kwa uchache watu laki moja na elfu 30 ya watu wanaoishi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu ni Mayahudi wenye asili ya Ethiopia ambapo kwa mujibu wa tovuti ya Ethiopian National Project, elfu 82 kati yao walizaliwa nje ya Israel.

 

Ukweli ni kwamba hali ya Mayahudi hao elfu 82 waliopelekwa katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu chini ya staratijia ya kuwahamishia wahajiri wa Kiyahudi huko Israel, inatofautiana sana na Mayahudi wengine wanaoishi ndani ya ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

 

Baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni linawatazama Mayahudi wenye asili ya Ethiopia na ambao wanaitwa 'Mafalasha', kuwa ni watu wa darala la tatu.

 

 

Ni kwa ajili hiyo ndio maana kunatekelezwa ukatili wa kimuundo dhidi ya Mayahudi hao wa Kifalasha, kukiwemo kuwabagua, kuwafanya kuwa masikini wa kutupwa na kuwafanyia ukatili wa kimwili.

 

Utawala wa Kizayuni ambao uliwapa ahadi mbalimbali Mayahudi hao wa Ethiopia kwa ajili ya kuwashawishi wahamie katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu, uliwaweka katika maeneo ya mashariki mwa Israel ambayo kwa kawaida huishi jamii za watu masikini.

 

Picha ya kijana aliyemiminiwa risasi bila hatia na askari wa Israel na kupelekea kuibuka maandamano

 

Mayahudi wenye asili ya Ethiopia na Mayahudi wanaotoka Mashariki wote wanalalamikia ubaguzi wanaofanyiwa na utawala huo wa Kizayuni. Kwa mfano, Mayahudi hao hawapewi haki sawa na Mayahudi wanaotoka nchi za Magharibi. Moja ya sababu za kuendelea maandamano ya Mayahudi wenye asili ya Ethiopia dhidi ya serikali ya Tel Aviv ni ubaguzi huo.

 

 

www.mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload