FAO: Idadi ya nchi zinazohitaji misaada ya chakula duniani imeongezeka

July 6, 2019

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza katika ripoti yake kwamba, idadi ya nchi zinazohitajia misaada ya chakula duniani imeongezeka.

 

 

Taarifa ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) imeeleza kuwa, idadi ya nchi zinazohitaji misaada ya chakula duniani imeongezekka na kufikia nchi 41.

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi 31 kati ya hizo 41 ni za Kiafrika na kwamba, migogoro ya muda mrefu na mazingira mabaya ya hali ya hewa kama ukame na kadhalika ni mambo ambayo yamechangia kuongezeka hitaji la misaada ya chakula. 

 

Mamilioni ya watu wanashindwa kupata chakula kutokana na vita, machafuko, migogoro ya muda mrefu katika nchi zao pamoja na ukame wa muda mrefu, imeeleza taarifa hiyo ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Nembo ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

 

Aidha kwa mujibu wa ripoti hiyo ya FAO ni kuwa, katika nchi nyingi barani Afrika zikiwemo, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati uhaba wa chakula umesababishwa na vita na machafuko ya muda mrefu.

 

Ripoti ya FAO inaeleza kuwa, Afghanistan, Bangladesh, Burkina Faso, Burundi, Cape Cerde, Cameroon, Chad, Korea Kaskazini na Congo Brazzaville ni miongoni mwa nchi nyingine zilizoko katika orodha hiyo ya nchi 41 duniani zinazohitaji misaada ya chakula kutoka nje.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon