Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Putin: Magaidi wanatorokea Libya, wanatokea Syria

July 5, 2019

Rais Vladimir Putin wa Russia ameonya kuwa, mgogoro wa kiusalama Libya huenda ukapanuka zaidi kutokana na wimbi la wananchama wa magenge ya kigaidi ambao wanatorokea nchi hiyo, wakitokea katika mkoa wa Idlib uliko kaskazini magharibi mwa Syria.

 

Rais Putin alitoa taadhari hiyo jana Alhamisi katika kikao na waandishi wa habari, baada ya kufanya mazungumzo na Giuseppe Conte, Waziri Mkuu wa Italia mjini Rome. 

 

Amesema, "Serikali ya Moscow inataka kuona pande hasimu za Libya zinasitisha mapigano na zinafanya mazungumzo, na kuingia katika mchakato halisi wa kisiasa utakaohakikisha kuwa changamoto zinazoikabili nchi hiyo zinapatiwa ufumbuzi."

 

Matamshi ya Rais wa Russia yametolewa siku chache baada ya ndege za wanamgambo wanaojiita "Jeshi la Taifa la Libya" wakiongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar kushambulia kituo cha kuhifadhia wahajiri walioingia kinyemela nchini Libya, karibu na mji mkuu Tripoli na kuua wahamiaji wasiopungua 60 na kujeruhi wengine zaidi ya 130. 

 

Tangu tarehe 4 Aprili mwaka huu na baada ya kutembelea Saudi Arabia, Jenerali Khalifa Haftar alitoa amri ya kushabulia mji mkuu wa Libya, Tripoli, ukatili unaoendelea hadi sasa ni kwa baraka kamili za Marekani ambayo hata ilikwamisha azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kulaani mauaji hayo ya wahajiri Libya.

Wanajeshi wa Syria wakipambana na magaidi mkoani Idlib

 

Mkoa wa Idlib unahesabiwa kuwa ngome ya mwisho kabisa ya makundi ya kigaidi yaliyovamia ardhi ya Syria kwa msaada wa nchi za Magharibi na washirika wao wa kikanda kama Saudi Arabia.

 

Juhudi zinazofanywa na jeshi la Syria na washirika wake za kutaka kukomboa eneo hilo zimekuwa zikikwamishwa na muungano wa nchi za Kiarabu na Kimagharibi zikiongozwa na Marekani kwa kutumia visingizio vya aina mbalimbali kwa shabaha ya kubakisha maficho ya magaidi katika eneo hilo.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload