Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jeshi, waandamanaji nchini Sudan wakubaliana kugawana madaraka

July 5, 2019

Wapatanishi wa Umoja wa Afrika wamesema majenerali wa kijeshi nchini Sundan wamefikia makubaliano na viongozi wa maandamano juu ya kugawana madaraka, katika mafanikio yaliofuatia wiki kadhaa za mkwamo wa kisiasa.

Makubaliano hayo ya kihitosria yamekuja baada ya siku mbili za mazungumzo, kufuatia kuvunjika kwa duru ya mwisho ya majadiliano mwezi Mei kuhusiana na nani anapaswa kuongoza chombo kipya cha utawala kati ya raia na jeshi.

 

"Pande mbili zimakubaliana kuunda baraza huru lenye uwakilishi sawa kati yao, jeshi na raia, kwa muda wa miaka mitatu au zaidi na pia wamekubaliana juu ya serikali huru ya kiraia, inayoongozwa na waziri mkuu msomi, ambayo itakuwa na uwezo na kutumikia taifa," alisema mpatanishi wa Umoja wa Afrika Mohamed El Hacen Lebatt katika mkutano na waandishi habari mjini Khartoum.

 

Sudan ametikiswa na mgogoro wa kisiasa tangu jeshi lilipomuondoa kiongozi wa muda mrefu Omar al- Bashir mwezi Aprili kufuatia maandamano ya umma dhidi ya utawala wale, ambapo majenerali waliotwaa madaraka walikataa matakwa ya waandamanaji kukabidhi mamlaka kwa utawala wa kiraia

Naibu kiongozi wa baraza la kijeshi Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, amesema makubaliano ya sasa hayambaguwi yeyote.

 

Mzozo kati ya pande mbili uliongezeka baada ya uvamizi wa kikatili dhidi ya kambi ya muda mrefu ya maandamano nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum uliosababisha vifo vya dazeni kadhaa za watu na kuwajeruhi mamia Juni 3.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload