Lindsey Graham: Bin Salman ndiye aliyetoa amri ya kuuliwa Jamal Khashoggi


Kwa mara nyingine seneta wa chama cha Republican nchini Marekani amesisitiza kuwa Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia ndiye aliyetoa amri ya kuuawa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa utawala wa Aal-Saud.

Lindsey Graham ameyasema hayo katika mahojiano na televisheni ya CBS na kuongeza kuwa, hakuna shaka kwamba Bin Salman ndiye aliyetoa amri ya kuuawa Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa uawala wa Saudia.

Aidha ameongeza kwamba Mrithi huyo wa Kiti cha Ufalme wa Saudia alikuwa na habari kamili kuhusiana na suala hilo kama ambavyo pia amewahi kufanya vitendo kama hivyo dhidi ya watu wengine.

Kwa mujibu wa seneta huyo wa chama tawala cha Republican nchini Marekani, Mohammad Bin Salman ndiye muhusika wa uharibifu katika eneo la Asia Magharibi.

Akiashiria muungano wa kistratijia kati ya Saudia na Marekani amesema: "Nimeamua kutofumbia macho shughuli za mshirika ambaye amemkatakata vipande mtu ndani ya ubalozi wake mdogo na kutozingatia sheria za kimataifa.''

Lindsey Graham, seneta wa chama cha Republican nchini Marekani.

Hata hivyo urafiki wa Trump na Bin Salman, unaivunjia itibari Marekani kuhusiana na suala la haki za binaadamu." Jamal Khashoggi, aliuawa kwa namna ya kutisha ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki tarehe Pili Oktoba mwaka jana.

Licha ya dunia nzima kumnyoshea kidole cha lawama Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia kuhusiana na mauaji hayo,

lakini Rais Donald Trump wa Marekani ameamua kufumbia macho suala hilo na kuendeleza urafiki na mtuhumiwa huyo. Katika uwanja huo, Trump amefafanua mara kadhaa kuwa, anazingatia hasa mikataba ya mauzo ya silaha na maslahi mengine juu ya masuala ya haki za binaadamu nchini Saudia.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu