Trump ametoa msimamo wake kufuatia kuaga dunia baba na binti yake wahajiri wa El Salvador

June 26, 2019

Rais Donald Trump wa Marekani ametoa kauli yake kufuatia kusambaa picha katika vyombo vya habari zinazomuonyesha baba na binti yake wa mwaka mmoja, ambao ni wahajiri wa El Salvador na waliofariki dunia kwa kuzama maji wakijaribu kuingia Marekani ambapo amewatwisha mzigo wa lawama wanachama wa Democrat na tukio hilo la maafa.

 

 

Akijibu swali la waandishi wa habari waliomuuliza nini msimamo wake kuhusiana na picha hizo, Trump amesema:

 

"Ninachukia kuona picha hiyo ya baba na mtoto wa kike, Lau kama Wademocrat wangebadili sheria, kuna uwezekano mkubwa kwamba yule baba asingekufa kifo kile pamoja na binti yake."

 

Amesema. Kuenea picha za miili ya baba mmoja muhajiri mwenye uraia wa El Salvador pamoja na binti yake katika ukingo ya Mto wa Rio Grande baada ya kuzama maji, kumeibua ukosoaji mkubwa kwa siasa mbovu za kuwabana wahajiri zinazotekelezwa na serikali ya Washington.

 

Inaelezwa kwamba raia huyo wa El Salvador alizama maji pamoja na mtoto wake wa kike wakati wakijaribu kuvuka mto huo kuingilia Marekani.

Baba na binti waliofariki dunia katika mto Rio Grande

 

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la nchini Uingereza, baanda ya baba huyo kufahamu kwamba familia yake haiwezi kuwaomba viongozi wa Marekani nchini Brazil kibali cha uhajiri, aliamua kuvuka mto wa Rio Grande unaopita kwenye mpaka wa Marekani. 

 

John Sanders, Kaimu wa Idara ya Forodha na Kulinda Mipaka ya Marekani amelazimika kujiuzulu cheo chake kufuatia kuenea kwa picha za kifo cha kutisha cha baba na binti wake kwenye mto huo.

 

 

Hata hivyo kujiuzulu huko hakukumpa umuhimu wowote rais wa Marekani. Aidha kuenea picha hizo za kutisha za wahajiri hao wa El Salvador kumezikasirisha fikra za walio wengi duniani kufuatilia hali mbaya ya wahajiri katika mpaka wa Mexico na Marekani..

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon