Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mbunge Jaguar wa Kenya aliyetaka kutimuliwa kwa wafanyabiashara wa kigeni atiwa mbaroni

June 26, 2019

Mbunge  wa Jimbo la Starehe jijini Nairobi nchini Kenya, Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ amekamatwa leo na jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda wanaoishi katika nchini hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Duru za habari mjini Nairobi zinasema kuwa, Jaguar amekamatwa nje ya ukumbi wa Bunge na kupelekwa kituo cha polisi ambacho hadi sasa bado hakijatajwa na jeshi hilo.

 

Awali serikali ya Nairobi kupitia Msemaji wa Serikali ya Kenya, Cyrus Oguna ilikuwa tayari imelaani kauli ya Jaguar na kueleza kuwa haikubaliki katika kipindi hiki cha utandawazi. “Wakenya ni watu wenye upendo na amani ambao kwa miaka mingi wameshirikiana na mataifa mbalimbali. Hii ni tunu tunajivunia na tutaendelea kushirikiana.”  Amesema Oguna.

Soko la Gikomba ambalo Jaguar alidai kutwaliwa na wafanyabiashara wa kigeni.

 

Serikali ya Kenya pia imewahakikishia usalama na ulinzi wageni wote wanaoingia na kuendesha shughuli zao za kibiashara nchini humo na kusisitiza kwamba, kauli ya mbunge Jaguar sio msimamo wa Kenya.

 

Jana katika mitandao ya kijamii Jaguar alionekana akizungumza maneno yenye vitisho kwa wageni kupitia kipande cha video kilichosambaa kuanzia siku ya Jumatatu.

 

Hata hivyo na kufuatia ukosoaji mkali, hatimaye mbunge huyo ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akidai kuwa, kauli aliyotoa ililenga raia wa China waliovamia biashara za Wakenya, suala ambalo bado liliendelea kukosolewa ndani na nje ya nchi hiyo.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload