Kim Jong-un asisitizia ulazima wa kuongezwa uwezo wa kujilinda wa nchi yake

May 4, 2019

Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini amesisitizia ulazima wa kuongezwa uwezo wa kujilinda wa jeshi la nchi yake kwa lengo la kujiweka tayari kwa ajili ya kulinda mamlaka ya kisiasa na kujitosheleza kiuchumi.

 

Kim Jong-un ameyasema hayo katika 'maneva ya ushambuliaji' ya kikosi cha wavurumishaji wa makombora, waongozaji wa silaha na mbinu, yaliyofanyika Jumamosi ya jana na kuongeza kuwa, jeshi la Korea Kaskazini linatakiwa kuinua kiwango chake cha uwezo kwa ajili ya kukabiliana na aina yoyote ya mazingira.

 

Aidha Kiongozi wa Korea Kaskazini amelipongeza jeshi la nchi hiyo kutokana na uhodari wake wa juu katika kuvurumisha makombora ya balestiki ya kisasa na pia ustawishaji wa silaha erevu na kimbinu, na hivyo amesifu mafanikio ya maneva hayo ambayo yamefanyika bila uratibu wa hapo kabla.

Kim Jong-un, akifuatilia shughuli za maneva hayo

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, 'maneva ya ushambuliaji'  ya Korea Kaskazini yaliyofanyika Jumamosi ya jana yalikuwa na lengo la kuchunguza uwezo wa kioperesheni, upimaji wa kiutendaji na uwezo wa kulenga shabaha wa uvurumishaji makombora wa kiwango cha juu kwa kutumia silaha erevu. Maneva hayo yalifanyika kwa usimamizi wa moja kwa moja wa Kim Jong-un.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon