Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Bin Salman amekaribia kuinunua klabu wa Manchester United ya Uingereza

May 4, 2019

Kwa mara nyingine tovuti ya habari za michezo ya Saudi Sport imesema kuwa, nia ya Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ya kuinunua klabu ya Manchester United ya nchini Uingrereza iko katika hatua zake za mwisho.

 

Itakukmbukwa kuwa, suala hilo lilizungumzwa sana pia mwishoni mwa mwaka jana 2018 lakini baadaye mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudia alikanusha.

Mfalme Salman na mwanawe viranja wa mauaji ya kikatili nchini Yemen

 

Katika miaka ya hivi karibuni, viongozi na matajiri wa koo za kifalme za nchi za Kiarabu wamekuja na wimbi kubwa la kununua vilabu vya mpira vya Ulaya. Vilabu vikubwa zaidi kununuliwa na watu wa koo hizo za kifalme ni Paris Saint-Germain ya Ufaransa na Manchester City ya Uingereza.

 

Watu hao wa koo za kiimla za kifalme za nchi za Kiarabu wanamwaga fedha nyingi sana kuendeshea vilabu hivyo.

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload