Maandamano makubwa dhidi ya Baraza la Kijeshi Sudan yanafanyika tena leo


Mandamano makubwa ya kulishinikiza Baraza la Kijeshi nchini Sudan likabidhi uongozi na madaraka ya nchi kwa raia yanafanyika leo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

Maandamano hayo yaliyoitishwa na muungano unaojulikana kwa jina la Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko yanataka Baraza la Kijeshi la Sudan likabidhi haraka mamlaka ya nchi kwa utawala wa kiraia.

Maandamano hayo yaliyoanza asubuhi ya leo katika mji mkuu wa Sudan Khartoum na miji mingine ya nchi hiyo

Muungano huo aidha umewataka wananchi wa Sudan kujitokeza kwa wingi Ijumaa ya leo kushiriki katika maandamano hayo ili kushinikiza kupatikane utawala wa kiraia.

Vikosi vya usalama nchini Sudan vinaonekana vikifunga baadhi ya barabara za mji mkuu Khartoum ili kuwazuia waandamanaji hao wasielekee upande wa Ikulu ya Rais.

Omar Hassan al-Bashir Rais wa zamani wa Sudan

Makundi ya kisiasa nchini Sudan yanalituhumu Baraza la Kijeshi la Mpito kwamba linakusudia kuendelea kushikilia madaraka kwa kisingizio cha kudhamini usalama wa nchi hiyo.

Baada ya kumpindua Rais Omar Hassan al-Bashir tarehe 11 mwezi Aprili, Baraza la Kijeshi la Mpito lilibuniwa na kuchukua madaraka ya nchi hiyo, lakini wanachi wamekuwa wakifanya maandamano ya kutaka madaraka hayo yakabidhiwe raia kutoka mikononi mwa wanajeshi.

Hali hiyo imeongeza mvutano kati ya baraza hilo na wananchi wanaofanya maandamano kila siku nchini humo wakitaka wakabidhiwe madaraka ya nchi haraka iwezekanavyo.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu