Onyo kali la Moscow dhidi ya uingiliaji wa kijeshi wa Washington nchini Venezuela

May 3, 2019

Katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Donald Trump wa Marekani, nchi hiyo imeongeza maradifu juhudi zake za kutaka kuiangusha serikali halali ya mrengo wa kushoto ya Venezuela inayoongozwa na Rais Nicolas Maduro.

Ili kufikia lengo hilo serikali ya Washington imezidisha hatua zake za kipropaganda na za vita vya kisaikolojia dhidi ya serikali ya Caracas kwa kuiwekea vikwazo vikali vya kiuchumi na hatimaye kutishia kuishambulia kijeshi. 

 

Katika uwanja huo, Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akizungumza Jumatano na kanali ya Fox News ya nchi hiyo aliitishia serikali halali ya Venezuela na kusema kuwa ikibidi, Washington iko tayari kuishambulia kijeshi nchi hiyo.

 

Kabla ya hapo pia Pompeo alidai kwamba Rais Maduro alikuwa yuko tayari kuikimbia nchi na kwamba ni Warussia ndio waliomzuia kufanya hivyo. Ameongeza kuwa licha ya hayo lakini vikwazo vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya nchi hiyo vimeilemaza kabisa.

 

Bila shaka vitisho hivyo vya Marekani dhidi ya Venezuela vimekabiliwa na radiamali kali ya Russia.

Katika mazungumzo yake ya simu na Mike Pompeo siku ya Jumatano, Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alimtahadharisha kuhusiana na matokeo mabaya ya kushambuliwa kijeshi Venezuela. Katika mazungumzo hayo ya simu, Lavrov alimwambia waziri mwenzake wa Marekani kwamba uingiliaji wa Marekani katika mambo ya ndani ya Venezuela ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na kwamba hujuma yoyote ya Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini itakuwa na matokeo mabaya mno.

Sergey Lavrov (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na mwenzake Mike Pompeo wa Marekani.

 

Kufuatia kushindwa jaribio la mapinduzi la hivi karibui nchini Venezuela ambapo Marekani imedhalilishwa wazi katika jaribio hilo la kijeshi dhidi ya Rais Maduro, Washington imeanzisha juhudii za kufunika aibu ya kushindwa huko kwa kueneza propaganda kuwa ni askari wa Russia walioko mjini Caracas ndio wamezuia ushindi wa waasi wanaoongozwa na Guaido.

 

Kwa msingi huo, Marekani inajaribu kupuuzilia mbali kwa makusudi nafasi na juhudi kubwa zilizofanywa na wananchi pamoja na jeshi la Venezuela, katika kuvunja njama na jaribio hilo lililofeli la mapinduzi siku ya Jumanne tarehe 30 Aprili.

 

 www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon