Rwanda yamkamata kinara wa kundi la waasi la NLF


Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa imemkamata mtu anayejitaja kuwa mkuu wa kundi la waasi la National Liberation Force (NLF)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Richard Sezibira amesema Rwanda imemkamata mtu anayejitaja kuwa mkuu wa kundi la waasi la NFL Callixte Nsabimana ambaye pia anajulikana kama Sankara.

Paul Rusesabagina,

NLF ni tawi la kijeshi la chama cha upinzani cha Rwanda Movement for Democratic Change (MRCD) kinachoongozwa na Paul Rusesabagina, anayefahamika kwa kuwaokoa watu kwenye Hoteli ya Des Mille Collines, wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Mwezi Julai mwaka jana Nsabimana alisema kuwa wameanza mapambano ya kisilaha ili kuiondoa madarakani serikali ya Rwanda.

Nsabimana amekuwa akitafutwa kutokana na makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuunda kundi la kisilaha, kuchochea vitendo vya kigaidi na makosa mengine.

Mwezi Disemba mwaka jana kundi hilo la NLF lilidai kuhusika na hujuma dhidi ya mabasi katika msitu wa Nyungwe karibu na mpaka wa nchi hiyo na Burundi ambapo watu wawili walipoteza maisha.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu