Adolf Hitler, dikteta wa Ujerumani anajiua mjini Berlin pamoja na mke wake Eva Braun -1945


Adolf Hitler ( alizaliwa Braunau, Austria, 20 Aprili 1889; na kufariki Berlin, Ujerumani, 30 Aprili 1945) alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake.

Alihutubia dharau na chuki ya kimbari dhidi ya watu wote wasio Wagermanik na hasa dhidi ya Wayahudi.

Alisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia na mateso ya watu milioni kadhaa. Akitangaza shabaha ya Ujerumani.

Gazeti la Marekani "Stars and Stripes" la tarehe 2 Mei 1945 latangaza kifo cha Hitler

Tarehe 30 Aprili Adolf Hitler aligawa sumu kwa wote waliokuwa pamoja naye katika boma chini ya ardhi akawaruhusu kuondoka; aliagiza sumu ijaribishwe kwa mbwa wake mpendwa "Blondi". Mnamo saa 15.30 Eva Brau alijiua kwa kumeza sumu na Hitler alijipiga risasi kichwani.

Wasaidizi wa mwisho walibeba maiti hadi bustani ya ikulu na kuziweka katika shimo kutokana na mlipuko wa bomu; hapa wakazichoma kwa petroli.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu