Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Kiongozi wa upinzani DRC awataka wananchi wamng'oe madarakani Rais Tshisekedi

April 30, 2019

Kinara wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewataka wananchi kutumia sauti na uwezo wao kumuondoa madarakani Rais Felix Tshisekedi wa nchi hiyo.

 

Martin Fayulu alitoa mwito huo  na kufafanua kuwa, "Nyinyi wananchi mna uwezo mkubwa kuliko jeshi lolote lile duniani. Katika nchi za Sudan na Algeria, wananchi waliungana na kuwang'oa madarakani marais wao. Hapa pia sisi lazima tufuate mkondo huo dhidi ya (Joseph) Kabila na (Felix) Tshisekedi."

 Fayulu amemtaja Tshisekedi kama mtu anayefedhehesha na ambaye aliwauza wananchi mkabala kwa maslahi yake ya kibafsi.

 Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Tshisekedi mshindi wa uchaguzi wa rais uliopita, kwa kupata asilimia 38.57 ya kura zote zilizopigwa huku Fayulu akiwa wa pili kwa asilimia 34.8. Mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary, aliambulia asilimia 23.8 na kuibuka wa tatu.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload