Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Kufanyika Kikao cha kwanza kati ya Kim Jong-un na Rais Vladmir Putin wa Russia

April 25, 2019

Jumatano Kim Jong-un Kiongozi wa Korea Kaskazini aliwasili nchini Russia kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza na Rais Vladmir Putin wa nchi hiyo.

 

Baada ya kuwasili mji wa Vladivostok  mashariki mwa Russia Jong-un amekutana na kufanya mazungumzo ya kufana na Rais Putin. Kabla ya kuanza safari hiyo Kim Jong-un alisema kuwa, alitaraji kwamba katika mazungumzo na rais huyo wa Russia wangeweza kujadili masuala muhimu kuhusiana na mgogoro wa Rasi ya Korea na kustawishwa mahusiano kati ya Moscow na Pyongyang.

 Ukweli ni kwamba safari ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini nchini Russia ni kwa ajili ya mazungumzo ya kistratijia na rais wa nchi hiyo, na ambayo imekuja baada ya kuvunjika kwa duru mbili za mazungumzo kati yake na Rais Donald Trump wa Marekani nchini Singapore na Vietnam na katika muda ulio chini ya mwaka mmoja uliopita, 

 Korea ya Kaskazini imetoa ujumbe kwa White House kwamba sasa Pyongyang inaelekea upande wa kustawisha uhusiano wake na Russia.

 

Hii ni katika hali ambayo kwa kuingia katika mazungumzo na Korea Kaskazini,

Baada ya Kiongozi wa Korea Kaskazini kuwasili mji wa Vladivostok wa mashariki mwa Russia hapo jana.

 

Trump alitarajia kwamba angeweza kuishawishi Pyongyang ifuate siasa na sera za Washington, jambo ambalo halikufanikiwa. Kutofikiwa mwafaka kwenye duru mbili za mazungumzo kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong-un,

 

kutokana na hali hiyo kumeifanya Korea Kaskazini ifikie hatua ya kusema  kwamba, Marekani ni nchi isiyoaminika na isiyo na itibari, ambayo licha ya Pyongyang kutekeleza makubaliano ya kusimamisha majaribio yake ya makombora na silaha za nyuklia, lakini haikuweza kutekeleza hata sehemu ndogo tu ya mapatano yao.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload