Mitandao ya kijamii kushitakiwa rasmi ikifanya uchochezi wa kigaidi

April 18, 2019

Bunge la Ulaya limepitisha  sheria ambayo itapelekea mashirika ya Facebook, Google na Twitter kushitakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria iwapo yataruhusu uchochezi wa kigaidi na misimamo mikali kubakia kwenye mitandao ya mashirika hayo.

Shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo na kusema kuwa, jana Jumatano, Bunge la Ulaya lilipitisha sheria ambayo kwa mujibu wake, mashirika ya Facebook, Google na Twitter yatalazimika kulipa fidia ya asilimia nne ya pato lao kama itapita saa nzima bila ya kufuta vitu vinavyochochea ugaidi na misimamo mikali vinavyotumwa na watumiaji wa mitandao hiyo ya kijamii

Bunge la Ulaya limepasisha sheria hiyo kwa kura 308 za ndio, 204 za hapana na 70 za kujizuia kupiga kura.

 

Bunge hilo limetangaza kuwa mashirika ambayo yatashindwa kuheshimu sheria hiyo yatalazimishwa kulipa fidia ya asilimia nne ya pato lao.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon