CNN: Marekani ndiye mnunuzi mkuu wa madawa ya kulevya

April 18, 2019

 Televisheni ya CNN ya nchini Marekani imesema kuwa serikali ya nchi hiyo ndiye mnunuzi mkubwa wa mihadarati na madawa ya kulevya yanayotoka eneo la Caribbean na Colombia.

 Katika ripoti yake, televisheni hiyo imesema kuwa, serikali ya Marekani ni mnunuzi wa kiwango kikubwa cha mihadarati hasa cocaine kutoka nchi za Colombia na za eneo la Caribbean.

 Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani ndiye mtumiaji mkuu wa madawa ya kulevya aina ya cocaine kuliko nchi nyingine yoyote ile duniani.

 

Uchunguzi wa siri uliofanywa na televisheni ya CNN unaonesha kuwa viongozi wa Marekani wanatambua vyema njia zinazotumiwa na kiwango cha magendo ya madawa ya kulevya yanayoingia nchini humo na kwa hakika jambo hilo linafanyika kwa ridhaa ya viongozi wenyewe wa Marekani.

 Ripoti hiyo imetolewa katika hali ambayo, hivi karibuni rais wa Marekani, Donald Trump, alikiri kwamba vijana wengi wa nchi hiyo wanatumia madawa ya kulevya.

 Takwimu rasmi zinaonesha kuwa, vifo vinavyotokana na matumizi ya aina mbalimbali za mihadarati vimeongezeka mno katika miaka ya hivi karibuni huko Marekani.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon