Watu 16 wauawa katika shambulizi la kuvizia nchini Nigeria


watu 16 wameuawa huku wengine 14 kujeruhiwa katika shambulizi la kuvizia lililofanywa na watu waliojizatiti kwa silaha katika eneo la Nasarawa magharibi mwa Nigeria

Msemaji wa Polisi wa Jimbo la Nasarawa, Umar Shehu Nadada, amewaambia waandishi wa habari kuwa, watu wasiojulikana walifanya shambulizi hilo katika kijiji cha Numa, ambapo mwanamke mjamzito ni miongoni mwa watu waliouawa.

Ameongeza kuwa, majeruhi wamepelekwa katika hospitali na zahanati za karibu, huku uchunguzi kuhusu kiiini na wahusika wa shambulizi hilo Nasarawa ukianza

Haya yanajiri wiki moja baada ya watu wengine 20 kuuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa, baada ya watu waliokuwa wamevalia magwanda ya kijeshi kushambulia kijiji kimoja katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria.

Mauaji hayo ya Kaduna yalijiri wiki moja tu baada ya watu 50 kuuawa katika shambulio jingine la wavamizi waliobeba silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Aidha mwezi uliopita, wavamizi waliokuwa juu ya pikipiki waliwaua kwa kuwapiga risasi watu 32 katika kijiji cha Kware, wilayani Shinkafi katika jimbo hilo hilo la Zamfara

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu