Bashar al Assad: Matatizo ya Mashariki ya Kati yanatokana na siasa mbovu za Marekani

April 17, 2019

Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa, moja ya sababu kuu za ukosefu wa amani Mashariki ya Kati ni siasa mbovu za Marekani za kuingilia masuala ya ndani ya nchi za eneo hili.

Bashar al Assad alisema hayo jana wakati alipoonana na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Damascus na huku akilaani hatua isiyokubalika hata kidogo iliyochukuliwa na Marekani dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, 

 amesisitiza kuwa, siasa za Marekani na za baadhi ya nchi za Magharibi haziwezi kuzizuia Iran, Syria na waitifaki wao kuendelea kupigania haki na manufaa ya mataifa yao.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hatua ya Marekani ya kutambua rasmi milima ya Golan ya Syria kuwa eti ni mali ya utawala pandikizi wa Israel na kuongeza kuwa,

 

hatua hiyo ya Marekani huwezi kuitofautisha na hatua yake dhidi ya Quds Tukufu na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, kwani hatua zote hizo zinaonesha kushindwa kwa siasa za Marekani katika eneo hili.

 Vile vile amesema, hatua za Marekani katika eneo la Asia Magharibi zimezifanya Iran na Syria zikurubiane zaidi katika masuala yote ya kieneo na kimataifa ikiwa ni pamoja na masuala ya usalama na utulivu wa eneo hili.

 

Baada ya ziara yake ya nchini Syria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana usiku aliwasili Ankara, kwa ajili ya ziara rasmi ya siku mbili nchini Uturuki.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon