Maafisa waudhibiti moto Kanisa la Notre Dame mjini Paris


Rais Emmanuel Macron ameahidi kulijenga upya kanisa kuu katoliki la Notre Dame mjini Paris ambalo jana jioni lilishika moto ulio unguza sehemu ya jengo.

Rais Macron ameeleza kuwa sehemu kubwa ya jengo haikushika moto ambao wakati mmoja ulitishia kuteketeza jengo zima na kuiacha Ufaransa ikiwa katika mshutuko kutokana na uharibifu wa jengo linaloelezwa kuwa alama ya nchi hiyo.

''Moto uliozuka jana jioni umeharibu paa llililojengwa miaka 850 iliyopita ambalo ni thurathi ya dunia.''

Mnara wa paa hilo uliteketea na kuanguka. Maafisa wapatao 400 wa zimamoto walihangaika usiku kucha kuuzima moto huo na hatimaye majira ya asubuhi walifanikiwa kuudhibiti na kulinusuru kanisa hilo zima lisiteketee.

Ujenzi wa kanisa la Notre Dame ulikamilika katikati mwa karne ya 12 baada ya miaka 200 ya kulifanyia kazi. Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa karne ya 18, kanisa hilo lilivamiwa katika vurugu dhidi ya kanisa katoliki na kuharibiwa.

Ajali hiyo imetokea katikati mwa matayarisho ya wiki takatifu kuelekea sikukuu ya Pasaka. Waumini kadhaa walionekana wakipiga mgoti na kusali wakati juhudi za kuudhibiti moto zikiendelea.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Audrey Azoulay amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa hisia kubwa zimezingira watu wanaoshuhudia kuungua moto kwa kanisa hilo ambalo UNESCO ililiorodhesha kama urithi wa dunia mwaka 1991.

Audrey Azoulay

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu