Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Raia wa Italia waandamana mbele ya bunge la EU kupinga mauaji ya raia wa Yemen

April 16, 2019

Kundi la wanaharakati nchini Italia limefanya maandamano mbele ya bunge la Umoja wa Ulaya kupinga mwendelezo wa mauaji dhidi ya raia wa Yemen unaofanywa na utawala wa Aal-Saud wa Saudia,

pamoja na washirika wake na pia kimya cha viongozi wa nchi za Magharibi kuhusiana na maafa yanayoshuhudiwa ndani ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu.

 

Katika maandamano hayo washiriki walifanikiwa kuingiza kwa dakika kadhaa kitambaa kilichoandikwa ujumbe wa maneno yanayosema, 'Komesheni Mauaji ya Raia wa Yemen' ndani ya ukumbi wa bunge hilo la EU.

 

Mmoja wa washiriki wa maandamano hayo amewaambia waandishi wa habari kwamba miaka miwili iliyopita bunge hilo ambalo ni nembo ya nchi za Ulaya lilitaka kusimamishwa mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia, lakini hadi sasa serikali za Ulaya ikiwemo Italia zimeendelea kuiuzia nchi hiyo ya Kiarabu silaha ambazo zinatumika katika kuwaua raia wa Yemen.

Kwa mujibu wa mwanaharakati huyo wa Italia ambaye hakutaka kutajwa jina lake, anasema serikali ya Italia kwa kushirikiana na shirika moja la Ujerumani linaloendesha shughuli zake ndani ya Italia, inazalisha mabomu na kuyatuma kwa siri kwenda Saudia.

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo miezi mitatu iliyopita kumejiri maandamano kadhaa mbele ya ubalozi wa Saudia mjini Rome, jengo la redio na televisheni ya nchi hiyo pamoja na ikulu ya rais ya kupinga mauzo ya mabomu ya Italia kwa Saudia.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload