Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Russia yakosoa vikali kitendo cha kutiwa mbaroni mwasisi wa mtandao wa kufichua siri wa WikiLeaks

April 11, 2019

Serikali ya Russia imekosoa vikali kitendo cha kutiwa mbaroni mjini London, Uingereza mwasisi wa mtandao unaojishughulisha na kufichua siri na kashfa wa WikiLeaks.

 

Dakika chache baada ya kusambaa habari ya kutiwa mbaroni na polisi wa Uingereza Julian Assange, mwasisi wa mtandao huo, Maria Zakharova, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametoa ujumbe akisema kuwa:

 

"Mkono wa demokrasia uko katika kukandamiza uhuru." Hayo yanajiri ambapo polisi ya Uingereza wametangaza kwamba, Assange alitiwa mbaroni Alkhamisi ya jana kwa amri ya viongozi wa Marekani na kwamba anaendelea kushikiliwa na vyombo hivyo vya usalama mjini London''.

Julian Assange, mwasisi wa mtandao huo baada ya kutiwa mbaroni

 

Taarifa iliyotolewa na polisi ya Uingereza imeongeza kwamba kutiwa mbaroni mtu huyo, kumejiri baada ya hukumu iliyotolewa mwaka 2012 na Mahkama Kuu ya nchi hiyo na pia baada ya serikali ya Ecuador kubatilisha kibali cha ukimbizi wa ulian Assange, mwasisi wa mtandao wa WikiLeaks, na hivyo ndipo polisi hiyo ikachukua hatua hiyo.

 

Assange alianzisha mtandao huo wa kufichua siri mwaka 2006, na mwaka 2010 sambamba na kusambaza video na picha za mauaji ya kutisha yaliyofanywa na askari wa Marekani nchini Iraq na Afghanistan, mtandao huo ukapata umshuhuri sana duniani. Aidha mwaka 2012 shakhsia huyo alikimbilia katika ubalozi wa Ecuador mjini London na kuomba kutambuliwa kama mkimbizi.

Rais Lenín Moreno wa Ecuador aliyetoa amri ya kukamatwa Assange

 

Hata hivyo Alhamisi ya jana Aprili 11, Rais Lenín Moreno wa Ecuador alibatilisha kibali cha ukimbizi wa Assange sambamba na kuwataka polisi ya Uingereza kuelekea kwenye ubalozi wa nchi yake mjini London na kumtia mbaroni mtu huyo.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload