Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Maandamano yashuhudiwa London baada ya kukamatwa mwasisi wa Wikileaks

April 12, 2019

 Maandamano yameshuhudiwa nje ya ubalozi wa Ecuador mjini London baada ya polisi ya Uingereza kumtia mbaroni mwasisi wa mtandao unaofichua fedheha nyingi za nchi na viongozi mbalimbali duniani wa WikiLeaks, Julian Assange, ambaye amekuwa akiishi ubalozini hapo tokea mwaka 2012.

Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yenye jumbe zinazosema, "Muachilieni huru Julian Assange", "Assange, mteule wa Tuzo ya Amani ya Nobel" na "Sisi ni Assange". Mmoja wa waandamanaji na mfuasi wa mwasisi huyo wa mtandao wa kufichua uozo serikali amesema, "Leo ni siku ya fedheha katika mfumo wa sheria wa Uingereza."

Julian Assange alikamatwa jana na maaafisa wa polisi wa mjini London, muda mfupi baada ya Rais wa Ecuador kubatilisha kibali cha kumpa hifadhi mwandishi huyo wa habari ambaye ameishi katika ubalozi wa Ecuador mjini London kwa miaka saba.

 

Wakili wa Assange, Jen Robinson amesema kuwa, mteja wake amekamatwa pia kutokana na ombi la Marekani ambayo inataka apelekwe nchini humo kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka ya kuvujisha nyaraka za serikali.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload