Licha ya Trump kumtaja Kim Jong-un kuwa ni rafiki yake, Pompeo amtaja kuwa ni mtu muovu

April 11, 2019

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, amemtaja Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini kuwa ni mtu muovu, licha ya kwamba rais wa Marekani, Donald Trump alimtaja kiongozi huyo kijana kuwa ni rafiki yake.

 

Pompeo ameyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na seneta mmoja wakati wa kikao cha bunge la seneti ya Marekani.

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya Pompeo kumtaja Rais Nicolás Maduro wa Venezuela kuwa ni mtu muovu aliulizwa swali juu ya iwapo sifa hiyo inamuhusu pia kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, alisema:

 

“Ninathibitisha kwamba nilishawahi kusema hivyo hapo kabla.” Weledi wa mambo wameyataja matamshi hayo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuwa yanaweza kutia doa uhusiano wa pande mbili za Washington na Pyongyang, hasa kwa kuzingatia kuwa hivi sasa Marekani inafanya juhudi kubwa za kuendeleza mazungumzo kati ya Trump na Kim Jong-un, baada ya kufeli mazungumzo ya mwezi Februari mwaka huu mjini Hanoi Vietnam.

Marekani imekuwa ikitumia mashinikizo na vikwazo kuilazimisha Korea Kaskazini isalimu amri mbele ya matakwa yake.

 

Siku chache zilizopita mjumbe maalumu  wa Korea Kusini katika Masuala ya Usalama na Amani ya Rasi ya Korea alinukuliwa akisema kuwa, Korea Kaskazini haitasalimu amri mbele ya vikwazo.

 

Lee Do-hoon alisisitiza kuwa, vikwazo haviwezi kuifanya Korea Kaskazini isitishe mpango wake wa silaha za nyuklia. Aidha alisisitiza kuwa, mazungumzo ya Marekani na Korea Kaskazini yanapaswa kuwa ya kina zaidi na yanayojadili masuala ya kimsing

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon