Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Kliniki ya macho Beni nchini DRC yasaidia manusura wa Ebola

April 10, 2019

Manusura wa Ebola akifanyiwa uchunguzi wa macho kwenye kliniki huko Beni, Jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia  ya Congo, DRC shirika la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Wizara ya afya pamoja na vyuo vikuu viwili kutoka Marekani wanasaidia manusura wa Ebola kujiepusha na ugonjwa wa macho.

 

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema manusura hao huko kwenye jimbo la Kivu Kaskazini wanakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uoni hafifu utokanao na kuwepo kwa uvimbe uchungu ndani  ya macho.

 Ili kukabiliana na matatizo kama hayo, Wizara ya Afya na WHO walianzisha kliniki ya macho kwenye mji wa Beni ambao ni kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ulioanza mwezi Agosti mwaka jana, kliniki ikiwa na vifaa vya kisasa zaidi.

 

Kliniki hii ya macho ni nyongeza ya kliniki zinazoendeshwa kwa mwezi mara moja kwa ajili ya manusura wa Ebola kwenye mji huo wa Beni pamoja na ile ya Mangina na Butembo tangu mwezi Novemba mwaka jana.

 

Dokta Jessica Shantha kutoka Chuo Kikuu Emory nchini Marekani anasema, “tunawachunguza wagonjwa mapema zaidi kuliko tulivyofanya awali. Inawezekana kuwa hawajapata huu ugonjwa. Kwa hiyo ni jambo ambalo wanapaswa kufuatiliwa kwa muda mrefu ili kuhakikisha hawapati tatizo au uvimbeuchungu kwenye macho. Na pia nadhani sote bado tunajifunza kutoka kwa manusura wa Ebola, ugonjwa wa macho na matatizo ya macho.”

 Catherine ni miongoni mwa wanufaika wa  huduma ya matibabu ya macho. Baada ya kuruhusiwa kuondoka kituo cha matibabu ya Ebola huko Beni mwezi Oktoba mwaka 2018,

 

Catherine akiwa naye hatarini kupata ugonjwa wa macho, alifika kituo na kupata huduma na anasema kuwa, “niliweza kuona kuwa walikuwepo pale kutupatia matibabu. Sikuhofia, nilielewa kuwa wanatibu macho yetu. Walikuwepo watu wengi wakiwemo wazungu.”

 Hivi sasa kuna manusura zaidi ya 300 wa Ebola ambao wamejisajili kupata matibabu ya macho.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload