Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mapinduzi ya kidijitali yasaidia kuinua uchumi wa baadhi ya nchi Afrika- Ripoti

April 8, 2019

Malipo ya miamala kwa njia ya kidijitali yanatumika sasa kuinua uchumi wa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Afrika.

 

Ripoti mpya ya Benki ya Dunia kuhusu uchumi kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara inasema kuwa ukuaji uchumi kwa nchi hizo umeendelea kuwa chini kwa mwaka wa nne mfululizo ikilinganishwa na ongezeko la idadi ya watu ingawa kiwango cha ukuaji uchumi kwa eneo hilo kwa mwaka huu wa 2019 kinatarajiwa kuwa ni asilimia 2.8.

 

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Benki ya Dunia iitwayo Pulse ambayo hupima hali ya chumi za Afrika mara mbili kwa mwaka.

 

Mathalani ripoti imesema kwa sababu za ndani na nje ya nchi hizo, kiwango cha ukuaji kwa mwaka jana kimelazimika kupunguzwa hadi asilimia 2.3 kutoka asilimia 2.5 mwaka uliotangulia wa 2017.

 

Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia kwa nchi za Afrika Albert Zeufack, akizungumzia ripoti hiyo amesema kasi ndogo inaakisi ukosefu wa uhakika kwenye uchumi wa dunia lakini “ndani ya nchi, ukosefu wa uhakika wa uchumi mkuu ikiwemo ongezeko la usimamizi dhaifu wa madeni, na mfumuko wa bei vimeshamiri kwenye mataifa mengi na vinaathiri uchumi wa Afrika.

Zaidi ya yote hali  ya utete inakwamisha ukuaji wa nchi za Afrika.”

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload