Wasiwasi wa Umoja wa Ulaya kuhusiana na hatua ya Marekani dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (I


Rais Donald Trump wa Marekani ambaye alishika hatamu za uongozi wa nchi hiyo Januari mwaka 2017, ameamua kuchukua mkondo wa kupuuza, kukosoa na kujiondoa Mahakama ya kimataifa.

Hadi sasa Marekani imeshajitoa katika asasi kadhaa zinazofungamana na Umoja wa Mataifa kama Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO na Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo;na katika hatua mpya, Washington imezitishia waziwazi asasi za kimataifa za mahakama.

Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani tarehe 15 ya mwezi uliopita wa Machi, alitishia kwamba, Washington itawanyima viza ya kuingia Marekani wale wote watakaojihusisha na uchunguzi tarajiwa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuhusiana na jinai dhidi ya wananjeshi wa Marekani nchini Afghanistan na kwamba, katu haitowaruhusu kuingia nchini humo.

Pompeo alisema bayana kwamba, serikali ya Marekani itatekeleza siasa za kubana viza kwa watu ambao watahusika moja kwa moja katika uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC mjini The Hague Uholanzi

Hatimaye Ijumaa iliyopita, Marekani ilitekeleza kivitendo tishio lake hilo baada ya kufutilia mbali viza ya kuingia nchini humo ya Fatou Bensouda Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. Bensouda amekuwa akisisitiza msimamo wake wa kutaka kufanyika uchunguzi kuhusiana na jinai za wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan.

Mkabala na hilo, Pompeo ametishia kuwa, endapo mahakama ya ICC itang'ang'ania msimamo wake huo wa kutaka kufanya uchunguzi kuhusiana na jinai za kivita za Marekani nchini Afghanistan, itasimamisha kwa muda viza za kuingia Marekani za wajumbe wengine wa mahakama hiyo.

Katika kipindi hiki cha kuweko huko Afghanistan, wanajeshi wa Marekani wamechukua hatua ambazo kwa mujibu wa sheria za kimataifa zinahesabiwa kuwa ni jinai za kivita na zinapaswa kufanyiwa uchunguzi na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC yenye makao yake mjini The Hague Uholanzi.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu