Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Ukosoaji mkali wa Rais Tayyip Erdoğan wa Uturuki kufuatia vitisho vya Marekani vya kuiondoa nchi hiyo katika NATO

April 7, 2019

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amekosoa vikali matamshi ya Mike Pence, Makamu wa Rais wa Marekani yaliyoashiria azma ya Washington ya kuiondoa Ankara katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO,

 

kutokana na sisitizo la viongozi wa Uturuki la kutaka kununua ngao ya makombora ya Russia.

 

Erdoğan alitoa radiamali hiyo siku ya Ijumaa kufuatia matamshi ya hivi karibuni ya Mike Pence dhidi ya Uturuki ambayo imeazimia kununua ngao ya makombora ya S 400 ya Russia na kuongeza kwamba matamshi hayo ni kosa kubwa.

 

Baadhi ya weledi wa masuala ya kijeshi wa nchi za Magharibi wanasisitiza kwamba, muda wa kuiondoa Uturuki ndani ya muungano wa NATO sasa umewadia.

 

Paul Valili, mtaalamu wa masuala ya kijeshi na jenerali mstaafu wa jeshi la Marekani ameieleza kanali ya televisheni ya Russia Today kwamba:

 "Siasa za Uturuki haziendi sawa na siasa za NATO na katika mazingira hayo chaguo la kuiondoa Ankara katika muungano huo ni linapewa kipaumbele hivi sasa."

 

Pamoja na hayo bado kuna vizingiti viwili vikuu vya kuweza kuiondoka Uturuki katika muungano huo.

 

Kizingiti cha kwanza ni kuwa, maamuzi yote ndani ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) huchukuliwa kwa namna ya mashauriano na baada ya kupigiwa kura ambapo Uturuki kama mwanachama inaweza kutumia kura ya Veto kukabiliana na aina yoyote ya maamuzi kma huo dhidi yake. Ama kizingiti cha pili ni hitajio kubwa la Umoja wa Ulaya kwa Uturuki.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload