Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Tafadhali tushikamane na waathirika wa kimbunga Idai:Wataalam UN

April 2, 2019

Wavulana wawili wakicheza kwenye maji ya mafuriko kufuatia kimbunga idai kupiga kambi ya wakimbizi ya Tongogara kusini mashariki mwa Zimbabwe.

 Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa,mjini Geneva Uswisi wametoa wito kwa mataifa, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi kuonesha mshikamano na nchi za kusini mwa Afrika baada ya kimbunga Idai kuwaua mamia na pia maelfu kubakia bila makazi huku pia kimbunga hicho kikisababisha hasara ya mabilioni ya fedha.

 Taarifa hiyo iliyochapishwa pia katika tovuti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR inaeleza kuwa hadi sasa, Idai imesababisha uharibifu nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi na kuwaua zaidi ya watu 700 ikiwa bado mamia hawafahamiki waliko. 

 

Watu wengine zaidi ya  milioni 3 wameathirika kuanzia tarehe 9 hadi 21 Machi 2019.

 

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa ni Obiora C. Okafor, mtaalamu huru wa haki za binadamu na mshikamano wa kimataifa, Bi Cecilia Jimenez-Damary mjumbe maalumu kuhusu haki za bindamu za wakimbizi wa ndani,

 

Bwana Léo Heller mjumbe maalumu kuhusu haki za binadamu kuhusu maji safi ya kunywa na usafi,

 

Bwana David R Boyd mjumbe maalumu wa haki za binadamu na mazingira, Bwana Saad Alfarargi, mjumbe maalumu katika haki ya maendeleo, Bwana Dainius Pῡras mjumbe maalumu katika haki ya afya ya mwili na akili,

 

 Bi Rosa Kornfeld-Matte mtaalamu huru katika kufurahia haki zote za binadamu kwa watu wenye umri mkubwa, Bwana Livingstone Sewanyana mtaalamu huru katika kuhamasisha utaratibu wa kidemkrasia na usawa wa kimataifa.

 

“Nchi zilizoathirika zinahitaji msaada ili kuunga mkono jitihada kadhaa ambazo zimeshafanywa na mashirika ya kiraia yakiwemo mashirika ya misaada wakati wa majanga ili kuleta nafuu kwa wale ambao wameathirika na masaibu yaliyosababishwa na kimbunga hiki.” Wamesema wataalamu''.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload