Bouteflika kunga'atuka mamlakani Aprili 28

April 2, 2019

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ataachia wadhifa wake huo Aprili 28, kabla ya kumalizika kwa muhula wake wa nne. Ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya washirika wake wa karibu kujitenga naye.

Ni hatua ambayo imechukuliwa katika wakati ambapo pia kuna maandamano makubwa ya raia ya kumshinikiza kiongozi huyo mdhaifu kung'atuka madarakani.

Maandamano  katika jiji la Algiers kumpinga Bouteflika

 

Bouteflika mwenye umri wa miaka 82, ambaye pia amekuwa akionekana mara chache hadharani tangu alipopatwa na kiharusi mnamo mwaka 2013, amekuwa akikabiliwa na wakati mgumu mamlakani, kutokana na kuongezeka kwa shinikizo kwa wiki kadhaa baada ya jaribio lake la kutaka kusalia madarakani baada ya miaka 20 ya utawala.

 

www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon