Ripoti zimeenea huenda rais Bouteflika wa Algeria akajiuzulu

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ametangaza serikali ili kutuliza malalamiko yaliyowatimua madarakani viongozi kadhaa hadi sasa.. Ripoti zinasema huenda mwenyewe Bouteflika akang'atuka wiki hii pia.

Vituo viwili vya kibinafsi vya televisheni, Ennahar na El Bilad vimetangaza uwezekano wa rais mkongwe na mgonjwa, Abdelaziz Bouteflika kujiuzulu wiki hii kufuatia maandamano ya umma na shinikizo la jeshi kumtaka asitishe utawala wake wa miaka 20.

Ripoti hizo zimetangazwa pia baada ya mkuu wa vikosi vya wanajeshi luteni jenerali Ahmed Gaid Salah kulitaka kwa mara nyengine tena baraza la katiba limtangaze rais Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 kuwa "hawezi kutawala."

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu